June 15, 2016

JOHN MABULA WAKATI AKIWA MTIBWA SUGAR, AKIMTHIBITI IDDI MOSHI MNYAMWEZI' WA YANGA.

Beki wa zamani wa Shinyanga Shooting na Mtibwa Sugar, John Mabula, anaangwa leo kuanzia saa nne kamili asubuhi nyumbani kwake Kitunda Kibeberu jijini Dar es Salaam.

Beki wa zamani wa Simba, Victor Costa Nyumba ambaye walicheza pamoja Mtibwa Sugar wamesema Mabula anaagwa leo na safari kwenda Shinyanga itaanza.

"Shughuli za mazishi zitafanyika nyumbani kwake Kitunda," alisema Costa.

Awali, shughuli za kuaga zilikuwa zifanyike jana, lakini ikashindikana na kusogezwa hadi leo.

Mabula aliuwawa kwa kushomwa kisu na mtu aliyekuwa akipigana na shemeji yake, yeye akaingilia kuamua. Baadaye mtu huyo alimuua na shemeji yake pia kumjeruhi mkewe.

Hadi sasa, Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, linaendelea kumtafuta mtu huyo.

Marehemu ambaye alichipukia kisoka katika timu ya Majengo mkoani Shinyanga, pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ kati ya miaka ya 2002-2004.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV