June 6, 2016


KOMBA
Baraza la Wazee la Yanga, limeamua kupeleka sauti za Mwenyekiti wa Uchaguzi  wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwenye makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Sauti hizo ni zile ambazo Alloyce Komba anatuhumiwa kwamba alikuwa akipanga mbinu za kumhujumu Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.

Taarifa za uhakika kutoka Yanga zinaeleza, wazee hao wakiongoza na katibu wao, Yahaya Akilimali watatua Takukuru leo kufanya kazi hiyo ili sheria ichukue mkondo wake.

 “Nimeambiwa na wazee wenzangu kwamba Jumatatu tunakwenda kufanya kazi hiyo ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake,” alisema mmoja wa wazee wa Yanga alipozungumza na SALEHJEMBE.


Tayari Komba ametangaza kukaa pembeni ili uchunguzi kupitia tuhuma hizo uchukue mkondo wake.

Uongozi wa Yanga uliahidi suala hilo litafikishwa kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV