July 9, 2016

PLUIJM
Moja ya tuzo zitakazokuwa na mvuto katika hafla ya utoaji tuzo za Ligi Kuu Bara ni ile ya kocha mkuu.

Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu.

 Makocha watatu ndiyo waliopewa nafasi ya kuwania tuzo hiyo na mshindi atajulikana hiyo Julai 17.

MAXIME

Makocha hao ni Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga (Tanzania Prisons). 

Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Pia kutakuwa na tuzo ya wamuzi bora katika kinyang'anyiro hicho ni Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV