July 10, 2016


Msemaji wa Simba, Haji Manara atapelekwa kati ya nchi hizi tatu, Ujerumani, Uturuki au India kwa ajili ya matibabu.

Manara amepata tatizo la jicho la kushoto ambalo aliamka likiwa haliona na inaonekana hata jicho lake la kulia limepunguza uwezo wa kuona.

Manara amesema baada ya kupokea vipimo, sasa anatakiwa kusafirishwa kwenda kupata matibabu zaidi.

“Tayari nimepata majibu na kila kitu kiko vizuri. Lakini matibabu zaidi yanaweza kufanya kati ya nchi hizo tatu.


“Naendelea kufanya uchunguzi wa mwisho na kujua wapi nitakwenda kwa ajili ya matibabu,” alisema Manara kwa sauti ya chini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV