July 10, 2016


Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limeitwanga Yanga faini ya dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 24) kutokana na utovu wa nidhamu.

Caf imeipiga Yanga faini kwa madai ya kupatikana na hatua ya kupoteza muda katika mechi dhidi ya Sagrada ya Angola wakati wa mechi ya mwisho kufuzu kucheza hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho.

Hata hivyo, Yanga itatakiwa kutanguliza kulipa dola 5,000 (zaidi ya Sh milioni 12. Halafu iliyobaki inaweza isilipe kama itaonyesha nidhamu bora hadi mwisho wa michuano hiyo.


Katika mechi ya pili ya nchini Angola, Sagrada iliifunga Yanga kwa bao 1-0. Lakini Yanga ikafuzu kutokana na ushindi wa mabao 2-0 jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV