July 9, 2016

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba leo ameonyesha kweli yeye ni Yanga damu baada ya kuibuka ghafla kwenye mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa kuivaa Medeama ya Ghana katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Mwigulu aliibuka katika mazoezi ya Yanga yaliyokuwa yakifanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani na kuwashangaza mashabiki waliokuwa hapo baada ya kuungana nao na kukaa chini kabisa.


Alikaa chini na kushuhudia mazoezi hadi mwisho, baada ya hapo alizungumza na mashabiki, makocha na wachezaji.
Alipozungumza na waandishi wa habari, Mwigulu aliyekuwa ametinga jezi za Yanga ‘full ngwamba’, alisisitiza suala la wachezaji kuendelea kujituma na kuwapa moyo.

“Wana uwezo kabisa wa kufanya vizuri, wasife moyo. Lakini kwa mashabiki tunapaswa kuonyesha Utanzania na kuachana na yale mambo ya kushangilia bendera ya Congo na kuiacha bendera ya Tanzania,” alisema Mwigulu ambaye ni mmoja wa washambuliaji wa kutumainiwa wa timu ya bunge.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV