July 9, 2016

KAIJAGE
Klabu ya Toto African ya Mwanza, rasmi imemtangaza Kocha Rogashian Kaijage kuwa kocha wake mkuu.

Kaijage aliyewahi kuinoa Twiga Stars anachukua nafasi iliyokuwa imeachwa na kocha mjerumani ambaye aliamua kuondoka na kurejea kwao.

Msemaji wa Toto, Cuthbert Angello ameithibitishia blogu hii kuwa Kaijage ndiye kocha mkuu mpya wa Toto.

SALEHJEMBE: Ni sahihi kuhusiana na Kaijage kuchukua nafasi ya kocha mkuu?
Angello: Ni kweli Kaijage anakuwa kocha mkuu.

SALEHJEMBE: Vipi kuhusu Tegete?
Angello: Hadi sasa ana mkataba na Toto, mkataba wa kocha msaidizi.

SALEHJEMBE: Mliona hafai kupandishwa na kuwa kocha mkuu?
Angello: Kamati ya utendaji imeona Kaijage anafaa kuwa kocha mkuu.

SALEHJEMBE: Tegete anabaki kuwa kocha msaidizi, au naye anaondoka?
Angello: Hilo litajadiliwa na kamati ya utendaji.

SALEHJEMBE: Kuna taarifa zinaeleza kwamba, kuna kocha msaidizi mpya anaajiriwa ndani ya siku chache?

Angello: Kamati ya utendaji haijanieleza kuhusu hilo, tuvute subira kidogo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV