July 8, 2016

 

Yanga imeendelea na mazoezi yake kujiandaa na mechi dhidi ya Medeama ya Ghana.

Mazoezi yaliyofanyika leo jioni kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Yanga walionekana wako vizuri na mazoezi yao yameendelea kuwa ya nguvu na kasi.

Yanga wana kibarua kigumu cha mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama, katikati ya wiki ijayo.

Kocha Hans van der Pluijm alionekana kuwa makini huku kila mara akisisitiza suala la umakini na kujiamini kwa kila kinachofanywa na wachezaji wake. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV