Baada ya uongozi wa Klabu ya Azam kuwasilisha barua kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka mechi zake zote za nyumbani watakazocheza dhidi ya Yanga na Simba, zipigwe kwenye uwanja wao wa Azam Complex, Yanga wameibuka na kusema wapo tayari kwa hilo.
Hivi karibuni Azam walifikisha barua hiyo ndani ya TFF baada ya kuona wananyimwa haki yao ya kuutumia uwanja huo kwa mechi zake za nyumbani wanazotakiwa kucheza na Yanga na Simba ambazo huwa zinahamishiwa Uwanja wa Taifa, Dar, hali ambayo hawataki kuona ikitokea msimu huu na kuendelea.
Kumekuwa na mjadala mkubwa baada ya Azam kupeleka barua hiyo ambapo wadau wamekuwa wakitofautiana kwa kusema ni sahihi kwa Azam kufanya hivyo huku wengine wakipinga.
Akilitolea ufafanuzi suala hilo jijini Dar, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, alisema wapo tayari kwenda kucheza kwenye uwanja huo endapo tu watahakikishiwa usalama wa kutosha kuanzia wachezaji, viongozi pamoja na mashabiki wao.
“Tunaweza kwenda kucheza kwao endapo tu makubaliano yakiafikiwa ambapo ni lazima kuwe na usalama wa uhakika, mbona Yanga tunacheza Morogoro, hapa kikubwa ni suala la usalama tu na wakituhakikishia hilo, hatuwezi kupinga,” alisema Baraka Deusdedit.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment