August 31, 2016

KESSY & MSUVA
Hassan Kessy beki wa kulia wa Yanga, Simon Msuva ni winga wa kulia wa Yanga. Kwa sasa katika kikosi cha Yanga chini ya Kocha Mholanzi, Hans van Pluijm.

Kessy amejiunga na Yanga msimu huu akitokea kwenye kikosi cha Simba kwenye usajili ambao ulizua utata mkubwa ambao mpaka sasa bado haujamalizika.

Hata hivyo ameshafanikiwa kucheza michezo mitatu kwenye timu hiyo, mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe na ule wa Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon.

Kessy alipata  nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza baada ya Juma Abdul kujitonyesha enka ameonekana akicheza kwa pamoja na ushirikiano katika mechi za hivi karibuni ameonekana kuelewana vizuri zaidi na pacha wake Simon Msuva.

Wachezaji hao, kwenye mechi na African Lyon walioonekana wakicheza kwa kuelewana kama wachezaji waliozoeana kucheza pamoja kitimu kutokana na aina yao ya uchezaji.

Wakati mechi hiyo inaendelea, Kessy alionekana akianzisha mashambulizi kwenye upande wake wa kulia akisaidiana na Msuva aliyekuwa akicheza juu yake yaani namba saba.

Kessy alionekana akibadilishana na Msuva kwa kubaki nyuma yake kwa ajili ya kukaba wakati wote akiwa uwanjani akiwa anaukokota mpira kwa ajili ya kwenda kupiga krosi kwenye goli la Lyon.

Wakati mechi hiyo ikiendelea, Msuva na Kessy kila mmoja alionekana akiyafanya majukumu ya mwenzake kwa ufasaha kwa beki kwenda kushambulia kwa kupiga krosi na winga kukaba wakati mwenzake anapokwenda kushambulia kwa kubaki chini yake.

Katika mechi hiyo, Msuva na Kessy walitengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao kwa kupiga krosi safi kwa washambuliaji wao Donald Ngoma na Amissi Tambwe ingawa nyingi washambuliaji hao walishindwa kuzitumia vyema.

Msuva, licha ya kutengeneza nafasi za mabao, lakini yeye mwenyewe alifanikiwa kufunga bao moja kwa kumchambua kipa wa African Lyon, Youthe Rostand akipokea pasi safi kutoka mbele kidogo ya katikati ya uwanja iliyopigwa na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.

“ Hawa jamaa wakielewana itakuwa hatari sana, wanaonekana kama vile wanaweza kufanya kitu cha tofauti kwenye kila mchezo.

“Kwanza wote wana kasi, halafu wote ni mafundi wa kupiga krosi, naona kama wanaweza kuisaidia sana Yanga msimu huu,” alisema kiongozi mmoja wa soka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, juzi.


1 COMMENTS:

  1. Faida tupu lakini Juma Abdul is still favourite!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic