September 2, 2016



Huku Simba wakienda Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupeleka ushahidi wa aliyekuwa beki wao, Hassan Kessy kuusitisha mkataba wake na timu hiyo, mwenyewe amepanga kuongeza program ya mazoezi binafsi ya gym.

Suala la Kessy, hivi karibuni lilichukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF huku ikijumuisha viongozi wa Yanga kwa ajili ya utetezi.

Wakati suala hilo likiendelea, beki huyo tayari ameruhusiwa na TFF kuanza kuitumikia Yanga inayonolewa na Mholanzi, Hans van Pluijm akiwa ameshacheza mechi tatu za timu hiyo.

Kessy amesema amepanga kujitenga na kufanya mazoezi ya kuongeza fiziki na fitinesi katika kujiweka fiti zaidi  ya alivyo hivi sasa.

“Kama unavyojua hadi kufikia suala hili linamalizika na mimi kuruhusiwa na TFF kuichezea Yanga, mengi yalitokea lakini nashukuru yameisha, hivyo nimepanga kuingia gym kwa ajili ya kuongeza ufiti.

"Ninataka niwe na stamina, kasi na pumzi za kutosha katika kupeleka mashambulizi kwenye lango la timu pinzani, hivyo ni lazima niwe fiti kuhakikisha ninaendana na kasi hiyo, gym ndiyo suluhisho la hilo," alisema Kessy.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic