September 2, 2016



Baada ya Kocha Mkuu wa Stand United ya Shinyanga, Patrick Liewig kudaiwa kumtolea maneno machafu msaidizi wake, Athuman Bilali ‘Bilo’ kwa madai kuwa alifanya mabadiliko uwanjani ya mchezaji Adam Kingwande badala ya Adam Salamba, uongozi wa timu hiyo umesema utamchukulia hatua kali Liewig kwa utovu wa nidhamu.

Tukio la Liewig kutibuana na Bilo lilitokea katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Stand United dhidi ya Kagera Sugar, wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Kambarage, mechi iliyomalizika kwa suluhu.

Katibu Mkuu wa Stand United, Kennedy Nyangi, amebainisha kuwa hiyo siyo mara ya kwanza kwa Liewig kuonyesha utovu wa nidhamu hadharani hasa dhidi ya wachezaji au benchi lake la ufundi, hivyo hawatamvumilia tena.


Mashuhuda wa tukio hilo wanasema lilitokea wakati mchezo ukiendelea ambapo ilionekana kama wanaigiza. Wahusika wote hawakupatikana kulizungumzia suala hilo.

Wakati akiwa Simba, Liewig pia alikuwa akilaumiwa kutokana na ukali uliopindukia, kufoka bila sababu za msingi huku wengine wakitaka avumiliwe kwa kuwa ni mtu mzima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic