October 18, 2016




Kampuni ya Multichoice Tanzania leo imetangaza huduma mpya ikiwa ni pamoja na kupunguza bei ya vifurushi vyake kwa wateja wa DStv.

Kuanzia Novemba Mosi, mwaka huu wateja wa DStv watanufaika na punguzo la bei katika vifurushi vya Premium, Compact Plus, Compact, Family na Access.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Multchoice Tanzania, Ronald Shelukindo amesema kuwa DStv Premium imepokea punguzo la asilimia 16 kuanzia Novemba Mosi ambapo bei yake mpya itakuwa ni Sh 184,000. Pamoja na hayo pia kifurushi hicho kitakuwa na ongezeko la chaneli nane.

 Kifurushi cha DStv Compact Plus kimepokiea punguzo la asilimia 17 na bei yake itakuwa ni 122,500.


“Chaneli hizo mpya zitarushwa na Vuzu, AMP, Lifetime, Discovery, Crime& Investigation, History na Africa Magic Showcase. Compact Plus imeongeza pia chaneli za michezo zitakazoendeleza msisimko kwa wapenzi wa soka kupitia vipindi vya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi za Ulaya na Europa na zote zitapatikana kwenye chaneli ya Supersport 6 na 4,” alisema Shelukindo.


Aidha, kwa wapenzi wa filamu za kiafrika watafaidi kupitia Nollywood, wapenzi wa tamthilia za Kilatini, wataburidika na Telenovelas, filamu za Bollywood na sinema zitakazopatikana kwenye chaneli za ROK, Eva Plus na B4U.

Kuhusu kifurushi cha Compact, bei yake mpya itakuwa ni 82, 250 ikiwa ni punguzo la 5%, kitakuwa na Ligi Kuu ya England, Premier na ile ya Ligi Kuu Hispania, La Liga lakini wateja wameongezewa chaneli za ITV Choice, TCM na Super Sport 4.


“Kwenye kifurushi cha Dstv Family, bei mpya ni 42,900 na kimepokea ongezeko la chaneli tano za B4U Movies, Eva, Eva Plus, Supersport 4 na Fox. Na kuhusu kifurushi cha Dstv Bomba, kuna ongezeko la chaneli tatu na bei yake mpya ni 19,950 kutoka 23,500,” aliongeza mkurugenzi huyo.


Hivi karibuni, DStv imekuwa ikiongeza wateja wake kwa kasi kubwa kutokana na punguzo la bei lakini matumizi ya Kiswahili katika vipindi vyake vipya.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic