October 22, 2016

OMOG KAZINI...
Kocha Joseph Omog wa Simba amethibitisha yeye ni bora kwani ameweka rekodi kwa kuwapoteza makocha wanne kutoka Ulaya kwa rekodi yake ya kutofungwa katika mechi 10 mfululizo za kwanza za timu hiyo.

 Omoga, raia wa Cameroon, ameweka rekodi hiyo kuanzia Agosti 20, mwaka huu alipoanza kuiongoza Simba dhidi ya Ndanda FC katika Ligi Kuu Bara ambapo Simba ilishinda mabao 3-1.

 Baada ya hapo, Omog aliiongoza Simba kushinda mechi nyingine saba, kutoka sare mbili na kutopoteza hata mechi moja hadi ile ya juzi Alhamisi ambapo iliifunga Mbao FC bao 1-0.

Rekodi hii ya Omog imewapiku makocha Wazungu walioifundisha Simba kati ya mwaka 2012 hadi sasa, kwani hakuna aliyeweza kucheza mechi 10 mfululizo za awali bila kufungwa.

 Kocha wa kwanza kuburuzwa na Omog ni Patrick Liewig raia wa Ufaransa ambaye katika mechi zake 10 ndani ya Simba kati ya Januari 25, 2012 na Aprili 15, mwaka huo alipata ushindi mara nane, akatoka sare moja na kufungwa mara moja.

 Aliyemfuatia Liewig ambaye amewahi kuinoa Stand United ni Zdravko Logarusic raia wa Croatia yeye aliiongoza Simba katika mechi 10 kati ya Januari 26, 2014 hadi Machi 30, 2014.

Logarusic alishinda mechi tatu tu, akatoka sare tatu na kupoteza mechi nne, huyu ndiye mwenye rekodi mbovu kuliko wenzake wote.

 Kocha mwingine ni Goran Kopunovic, raia wa Serbia, yeye katika mechi zake 10 za kwanza alizoiongoza Simba kati ya Januari 17, 2015 hadi Machi 14, 2015, alishinda sita, akatoka sare mbili na kufungwa mbili, lakini ndiye aliyeifunga Yanga kwa bao la Emmanuel Okwi dakika ya 54, Machi 8, 2015.

 Dylan, Kerr raia wa Uingereza, yeye katika mechi zake 10 za kwanza Simba kati ya Septemba 12, 2015 hadi Desemba 12 mwaka huo, alishinda saba, akatoka sare mbili na kufungwa mara moja.

Lakini Omog amesema yeye haangalii masuala hayo ya rekodi, anachotaka ni kuiongoza Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

“Nitaendelea kupambana kuhakikisha Simba inafanya vizuri zaidi na hata Jumapili (kesho) dhidi ya Toto. Ni mechi ngumu lakini tutapambana,” alisema Omog.

MECHI 10 ZA  SIMBA:
Simba          3-1         Ndanda
JKT Ruvu     0-0         Simba
Simba          2-1         Ruvu Shooting
Simba          2-0         Mtibwa
Azam FC      0-1         Simba
Simba          4-0         Majimaji
Yanga          1-1         Simba
Mbeya City 0-2           Simba
Simba          2-0         Kagera Sugar

Simba          1-0         Mbao

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic