October 17, 2016


Beki wa Azam FC, Shomari Kapombe, amepewa wiki mbili za kuwa nje akiuguza jeraha lake la goti wakati beki kisiki Muivory Coast, Pascal Wawa yeye anaendelea kula bata kutokana na kutengewa muda wa kupumzika zaidi licha ya kupona.

Kapombe ambaye amekuwa mhimili mkubwa wa Azam inayofundishwa na Mhispania, Zeben Hernandez katika beki ya kulia, alipata majeraha hayo wiki chache wakati alipokuwa anaitumikia timu hiyo kwenye moja ya mechi zake.

Msemaji wa Azam, Jaffar Idd, amesema kwa mujibu wa ripoti ya benchi la utaratibu wa timu hiyo Kapombe amepewa muda huo kwa ajili ya kupona kabisa goti lake kabla ya kurejea uwanjani kuipigania timu hiyo ambayo imekuwa na matokeo ya kusuasua.

“Kwa sasa Kapombe yeye amepewa muda wa wiki mbili na madaktari wa timu ambazo atazitumia siku hizo kwa ajili ya kujiweka sawa na kupona jeraha la goti ambalo alilipata hivi karibuni.


“Lakini kwa upande wa Wawa licha ya kupona tatizo lake la nyama za paja bado hayupo kwenye timu kwa sababu anapewa muda zaidi wa kupumzika kutokana na kutumika kwa kiwango kikubwa msimu uliopita na baada ya muda mfupi ujao atajiunga na wenzake,” alisema Idd.

SOURCE: CHAMPIONI  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic