October 15, 2016

MWANJALE ALIPOTUA SIMBA
Kikosi cha Simba kinaongoza Ligi Kuu Bara lakini kimekuwa jeuri kwa kusema inaweza kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu kutokana na usajili makini ilioufanya ukiwemo wa Shiza Kichuya na Method Mwanjale.

Meneja wa Simba ambaye pia ni straika wa zamani wa timu hiyo, Mussa Mgosi, amesema wana kila ya sababu ya kuuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu, kwani wamesajili wachezaji wanaoweza kupambana.

Kauli hiyo ya Mgosi imekuja baada ya Simba kucheza mechi nane hadi sasa na kufikisha pointi 20 huku ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja, kwani ina sare mbili na imeshinda mara sita.

Ukiachana na Kichuya na Mwanjale, msimu huu Simba pia imewasajili Muzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Jamal Mnyate, Mousa Ndusha, Besala  Bokungu, Mohamed Ibrahim, Malika Ndeule, Fredric Blagnon na Hamad Juma ambao wameonekana kutoa msaada mkubwa kikosini.

Mgosi alisema: “Msimu huu tumetengeneza wigo mpana wa kikosi bora ambacho kimeleta ushindani wa namba kwa wachezaji wenyewe.

“Kutokana na hali hii, tuna matumaini makubwa ya kuuchukua ubingwa msimu huu.”

Mgosi alisema, wigo huo mpana wa kikosi umesababisha kutokuwepo kwa mchezaji tegemeo katika timu, hivyo  mtu akiumia basi kunakuwepo na mbadala wake mwenye uwezo kama aliyetoka.

Aliongeza kuwa, hivi sasa ni jukumu la viongozi na mashabiki kwa pamoja kuungana kuisapoti timu yao ili waipokonye ubingwa Yanga kwenye msimu huu wa ligi kuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic