October 20, 2016

MAXIME


Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, amesema kikosi chake hakitakuwa tayari kuiachia Yanga kuondoka na pointi zote tatu watakapokutana mjini Bukoba.

Maxime amesema katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Jumamosi, itakuwa ngumu na wao wanataka faida.

“Tuko nyumbani kwetu, tunajua Yanga ni timu nzuri lakini tunataka kushinda,” alisema.

“Waje tu lakini kweli tunahitaji pointi, ziwe tatu au moja lakini tunahitaji pointi.”

Kagera ni moja ya timu zinazofanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara, iko katika nafasi ya nne baaada ya kucheza mechi 11 na kukusanya pointi 18.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV