October 20, 2016Kocha wa Simba, Joseph Omog amewataka wachezaji wake kufanya mambo mawili watakapokutana na kikosi cha Mabao FC.

Simba inakutana na Mbao FC katika mechi ya Ligi kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Omog amewataka wachezaji wake kutodharau, pili kupata mabao mapema.

“Kochaa amesisitiza sana suala la dharau, hakuna haja ya kuwa dharau Mbao kwa kuwa ni timu iliyopanda daraja na badala yake tunachotakiwa ni kufanya kazi yetu kwa ufasaha.

“Pili amesisitiza tufunge mapema, unajua kabla timu yetu ilikuwa inapata mabao kipindi cha pili tu, sasa tumebadili hilo,” alisema mmoja wachezaji wa Simba.


Simba ndiyo inaongoza ligi hiyo kwa kuwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 9.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV