October 21, 2016


Huku Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, akiwaongoza wenzake kadhaa kupinga ukodishwaji wa timu hiyo, wazee wengine wa klabu hiyo wa jijini Mwanza nao wameibuka wakidai kuwa wanataka timu ikodishwe ili ipate maendeleo.

Yanga ipo katika mvutano baada ya Mwenyekiti Yusuf Manji kutoa ombi la kutaka kukodisha timu hiyo na nembo yake kwa miaka kumi, jambo ambalo limekuwa na mvutano mkubwa.

Wazee wa Mwanza wamezungumza na kusema mabadiliko ni muhimu kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, hivyo suala la kuwekeza klabuni halikwepeki kwa sasa.

Mwenyekiti wa Wazee Tawi la Mwanza, Felix Felishiana, alisema wazo la mwenyekiti huyo linatakiwa kuheshimiwa na kufanyiwa kazi hasa katika kuleta maendeleo ya timu kwani maendeleo yaliyopo hivi sasa katika timu hiyo, yanatokana na mchango mkubwa wa mwenyekiti huyo.

Felishian alisema wazee wa Yanga Tawi la Mwanza wanamuunga mkono mwenyekiti wao kuikodisha timu hiyo kwa miaka 10 na kuwataka wanachama wengine ambao wanaleta vipingamizi kuhusu suala hilo kuacha kwani wanachelewesha maendeleo ya timu hiyo.


“Sisi tunamuunga mkono mwenyekiti wetu, Yusuf Manji kuikodisha timu, hata mafanikio tuliyonayo hivi sasa yanatokana na mchango mkubwa ambao mwenyekiti wetu ameutoa,” alisema Felishian.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV