Mshambuliaji mpya wa AFC ya Sweden, Mtanzania Thomas Ulimwengu ameendelea kujifua vilivyo kuhakikisha anaanza kazi akiwa vizuri.
Tayari amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo na sasa yuko jijini Barcelona nchini Hispania ambako wamekwenda kwa ajili ya kambi.
Ulimwengu si mgeni nchini Sweden wala klabu ya AFC ambayo ndiyo ilimuuza kwa TP Mazembe akitokea katika kikosi cha vijana cha klabu hiyo inayomilikiwa na milionea wa Kirusi.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe ni kati ya wanaopewa nafasi ya kung’ara katika ligi hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment