January 27, 2017
Beki wa kati wa Simba, Juuko Murshid, ameambiwa anatakiwa kurejea mapema nchini kutoka Gabon alikoenda kushiriki michuano ya Kombe la Afrika (Afcon) ili ikiwezekana awahi mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Azam FC, kesho Jumamosi.

Juuko alikuwa akiitumikia Uganda katika michuano hiyo, hivyo kukosa mechi kadhaa za klabu yake lakini Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, amesema beki huyo anatakiwa kurejea kuendelea na majukumu yake licha ya awali kuwepo na taarifa kuwa mchezaji huyo hana mpango wa kurejea Simba.

“Juuko wakati wowote anatarajiwa kutua nchini ndani ya wiki hii, ninaamini kabla ya mechi ya Azam atakuwepo nchini,” alisema Omog. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV