Katika hali isiyokuwa ya kawaida, hali ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, imeendelea kuwa mbaya baada ya majani ya uwanja huo kukauka kutokana na idara ya maji safi na maji taka kukata huduma ya maji katika uwanja huo kutokana na deni wanalodaiwa wamiliki wake.
Meneja wa uwanja huo, Steven Shija, amenukuliwa akisema: "Ni kweli uwanja hali yake siyo nzuri, hii inatokana na idara ya maji kukata maji hapa uwanjani, hivyo tukakosa namna ya kuumwagilia lakini tumeshalipa deni tulilokuwa tunadaiwa na sasa tutaanza kuumwagilia ili urudi katika hali yake kama zamani.
"Baada ya kulipa deni, kuna kifaa kitaletwa kwa ajili ya kuruhusu maji kuingia ndani na yakishaingia tutaumwagilia uwanja huu usiku na mchana ili haraka uweze kurudi katika hadhi yake.”
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment