Dakika ya 90 + 4: Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga wanaibuka na ushindi wa bao 1-0.
Dakika ya 90 + 1: Yanga wanafanya shambulizi lakini Msuva anakosa nafasi.
Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 4 za nyongeza.
Dakika ya 90: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Niyonzima, anaingia Oscar Joshua. Kabla ya kutoka Haruna kakabidhi kitambaa cha unahodha kwa Yondani.
Dakika ya 89: Baadhi ya mashabiki wameanza kutoka nje ya uwanja kuonyesha kuwa wamekata tamaa na matokeo yatakuwa kama yalivyo.
Dakika ya 87: Tambwe anapelekwa nje kupatiwa matibabu, mpira unaendelea.
Dakika ya 86: Tambwe anachezewa faulo mara mbili katikati ya uwanja na mara zote mwamuzi anapuliza kipenga.
Dakika 85: Mchezo umetawaliwa na ubabe wa hapa na pale.
Dakika ya 80: Deusi Kaseke wa Yanga anatoka anaingia Said Juma Makapu.
Dakika ya 75: Mchezo bado ni mgumu na timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 70 Majimaji wanarejea tena langoni kwa Yanga lakini Dida anauwahi mpira na kuudaka.
Dakika ya 68: Majimaji wanatengeneza shambulizi lakini Yondani anawahi na kuokoa.
Dakika ya 64: Msuva anachezewa faulo katikati ya uwanja mwamuzi anapuliza kipenga. Juma Abdul anapiga faulo hiyo mpira unadakwa na kipa wa Majimaji.
Dakika ya 62: Yanga wanafanya shambulizi kali, Msuva anashindwa kutumia nafasi anayopata akiwa mbele ya lango la Majimaji.
Dakika ya 59: Majimaji wanafanya mabadiliko, anatoka Yakub Abdallah anaingia Paul Nyangwe.
Dakika ya 57: Mchezo unaendelea.
Dakika ya 56: Yondani ameumia na mchezo umesimama kwa muda akipatiwa matibabu.
Dakika ya 51: Yanga wanapiga faulo lakini kuna wachezaji wanaotea.
Dakika ya 48: Emmanuel Simwanza anapata kadi ya njano kutokana na kumvuta jezi Msuva. Yanga wanapata faulo nje ya lango la Majimaji.
Dakika ya 47: Timu zimeanza kusomana na kasi siyo kali kama ilivyokuwa awali lakini shangwe za mashabiki ni kubwa na wanaendelea kushangilia kwa nguvu pande zote, wale wa Majimaji na wa Yanga.
Kipindi cha pili kimeanza.
Timu zinaingia uwanjani kuanza kipindi cha pili.
Dakika ya 45 + 2: Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 44: Licha ya kuwa nyuma kwa bao moja lakini Majimaji wanaonekana kutokata tamaa. Wanapata faulo baada ya Juma Abdul kumchezea faulo beki wa Majimaji katikati ya uwanja.
Dakika ya 40: Mchezo umekuwa ni wa kushambuliana zamu kwa zamu.
Dakika ya 37: Majimaji wanajipanga tena lakini wanapokwa mpira, Yanga wanapiga pasi ndefu kwa Mahadhi, anampa Niyonzima, anapiga krosi. Tambwe anautupia mpira wavuni lakini anakuwa ameotea.
Dakika ya 36: Majimaji wanafanya shambulizi kwa kupiga shuti la mbali lakini Dida anawali na kuokoa.
Dakika ya 33: Majimaji wanaendelea kujipanga lakini wanashindwa kujipanga vizuri wanavyokaribia lango la Yanga.
Dakika ya 30: Kasi ya mchezo imepungua kidogo, jua ni kali kwenye eneo hili la Uwanja wa Majimaji, idadi ya mashabiki nao ni wengi.
Dakika ya 28: Majimaji wanafika langoni kwa Yanga lakini kipa Dida anauwahi mpira.
Dakika ya 25: Majimaji wanafanya mabadiliko, anatoka Bahati Yusuph anaingia Emmanuel Simwanza.
Dakika ya 24: Majimaji wanaonekana kutulia na kutokuwa na papara lakini Yanga wanamiliki mpira muda mwingi, mchezo bado una kasi ingawa Yanga wanaonekana kupunguza kidogo baada ya bao.
Dakika ya 21: Beki wa Yanga, Kelvin Yondani anaonyesha hataki utani, mpira ukielekea eneo lake anaupiga kwa nguvu.
Dakika ya 18: Majimaji wanaonekana kuanza kuamka na kutengeneza mashambulizi.
Niyonzima alipiga krosi kutoka upande wa kushoto, kipa wa Majimaji akaipangua, Kaseke akakutana na mpira na kupiga shuti kali, lililojaa wavuni.
Dakika ya 14: Yanga wanapata bao kupitia kwa Deus Kaseke baad aya kazi nzuri iliyofanywa na Haruna Niyonzima.
Dakika ya 14: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!
Dakika ya 10: Kasi ya mchezo inaendelea na inaonekana Yanga wanatafuta bao la mapema.
Dakika ya 7: Simon Msuva wa Yanga anapata nafasi anapiga shuti kali kutoka upand wa kulia, linapaa juu kidogo ya lango.
Dakika ya 5: Mchezo unaendelea kwa kasi huku timu zote zikijipanga.
Dakika ya 2: Yanga wanafanya shambulizi kali langoni mwa Majimaji, Amiss Tambwe anaingia na mpira, anakutana na kipa wa Majimaji ambaye anafanya kazi nzuri kuupangua na kuwa kona.
Dakika ya kwanza: Mchezo umeanza.
Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuanza kwenye Uwanja wa Majimaji, kati ya wenyeji Majimaji FC dhidi ya Yanga
0 COMMENTS:
Post a Comment