February 2, 2017



Baraza la Wazee la Klabu ya Simba na uongozi wa klabu wamefikia mwafaka wa kufanya kazi pamoja kwenda katika mabadiliko.

Awali, kulikuwa na hali ya kutoelewana huku baadhi wakipinga Simba kuingia kwenye mabadiliko ambayo yangemuwezesha bilionea kijana Afrika, Mohamed Dewji ambaye aliweka ofa ya Sh bilioni 20 kunuua hisa asilimia 51.


 Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais wa Simba,  Evans Aveva alisema sasa wao na baraza la wadhamini wako pamoja.

“Siku za karibuni kulikuwa na maneno mengi  yakisemwa kwamba uongozi  hauna maelewano mazuri na wadhamini ambao ni walezi na wenye mali, napenda kuwataarifu  kwamba tumekuwa na vikao na vya mara kwa mara hata juzi (Jumatano) tulikuwa na kikao cha mwisho kuangalia tunafanya nini  katika klabu yetu ya Simba.


 “Leo hii nimekuja na mwakilishi wa Baraza la Wadhamini wa Simba, mzee wetu Hamis Kilomoni ili kuweza kuwaambia kuwa sasa tunataka kukufanya kazi ya kuletea maendeleo klabu yetu,”alisema Aveva.

Akilizungumzia suala hilo, mzee Kilomoni alisema walikaa pamoja na mwisho wakaamua kutoa tamko.

“Tumeyazungumzia haya yote yaliokuwa yanatokea na ndiyo maana tulitoa tamko. Anayekosoa na kuomba msamaha ni mwema, lengo tuone ipi ni njia sahihi.

 “Kwa wanakumbuka, Simba ilianza 1936 na nimeitumika kwa muda mrefu hivyo ukianza kutokea mgawanyiko hivi sasa hakutakuwa na maana yoyote.

Kutokana na hatua waliyofikia, huenda ikasaidia kufanikisha mchakato wa suala hilo.



1 COMMENTS:

  1. Hapo uongozi Simba mmefanya jambo zuri sana,Sasa waombe hao ukawa wakupe watu watano wazee wa kazi uwajumuishe kwenye kamati ya ufundi nje ya uwanja.Unda kamati ya kulinda na kufuatilia kwa karibu viwango vya wachezaji ili kuwabaini wachezaji wanaowapiga misumari wenzao ili waonekane wao tu,huko nikuihujumu timu,na hicho kitu kipo sana bongo hasa wazawa dhidi ya wageni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic