Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ameonekana kulifurahia jina la Donald Triump alilobandikwa na mashabiki.
Mashabiki wa Simba wamempa Dalali jina la Triump wakimfananisha na Rais wa sasa wa Marekani, Donald Triump.
“Kweli nimesikia kuhusiana na jina hilo, lakini sina namna ya kufanya.
“Unajua hata Field Marshal, mashabiki walinitunga wao. Mwanzo niliona kama halitaendelea. Lakini mwisho likawa maarufu sana.
“Siwezi kuwakatalia, wala siwezi kulaumu. Badala yake nafurahi,” alisema Dalali.
Hata hivyo, Dalali amekuwa kimya kwa muda mrefu akiwa haonekani kujihusisha na masuala ya soka.
“Hapa katikati niliumzwa sana. Lakini sasa nimepata nafuu, naweza kusema nimepona na baadaye nitaendelea na mambo yangu lakini nikuhakikishie bado nipo kwenye soka.”
0 COMMENTS:
Post a Comment