February 1, 2017



Unaweza kusema kweli hali ya uchumi ni ngumu na klabu ya Yanga, imeamua kupitisha “fagio la chuma” ili kufanya punguzo la wafanyakazi wake kwa lengo la kuweza kuendelea kujiendesha.


Kati ya wanaoondoka katika orodha ya watumishi wa Yanga ni Mkurugenzi wa Habari wa klabu hiyo, Jerry Cornel Muro ambaye amekuwa akiendesha kipindi cha runinga katika runinga ya ITV na uchambuzi katika Gazeti la Namba Moja la Michezo nchini la Championi.

Mkataba wa Yanga na Muro umemalizika Desemba, mwaka jana. Tokea hapo, Yanga haikuwa imemuongezea mkataba. Na imeonekana anapaswa kuingia kwenye orodha hiyo kwa kuwa kati ya wale wasio na mchango mkubwa kwa sasa.

Muro amefungiwa mwaka mmoja na SHirikisho la Soka Tanzania (TFF), hivyo amekuwa hazungumzi lolote kuhusiana na Yanga.



Taarifa kutoka ndani ya kamati ya utendaji zimeeleza kuwa, Katibu Mkuu mpya wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ndiye atakayetoa taarifa kwa wafanyakazi kumi na moja ambao wamekumbwa na “fagio la chuma”.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, amesema uongozi tayari umewasiliana nao na wameridhia.

“Kweli na ninakuhakikishia, uamuzi wa uongozi ni kubana matumizi zaidi. Hivyo tunachokifanya hapa kwa pamoja kamati ya utendaji na uongozi ni kuangalia hali ilivyo,” kilieleza chanzo hicho.

“Unajua Yanga inakwenda kwa hasara, mechi kuonyeshwa kwenye Azam TV ni tatizo kubwa kabisa. Hakuna tunachopata na sasa imefikia tunashindwa kulipa mishahara. Wako ambao wanajikaza hawasemi ukweli, lakini siku itafika tu hawatavumilia haya maumivu.

“Najua suala la Muro litawashitua watu wengi. Lakini Ni mtu mwenye kazi yake kwa kuwa ni mtaalamu wa masuala ya habari. Kila mjumbe wa kamati anajua na hii ni kwa ajili ya nia njema kwa klabu na wote tumeridhia.

“Tunafanya hivi ili kuweza kuendelea kuwalipa wachezaji na wafanyakazi wengine. Ingekuwa mambo ni mazuri, hakuna ambaye angeondolewa.”

Pamoja na Muro, “panga” hilo limepita kwenye vitengo vya fedha, masoko, usafi na ulinzi.

Mmoja wa waliokumbwa na “panga” hilo ni bwana fedha, Faidhal Mike ambaye nafasi yake inachukuliwa na Baraka Deusdedit aliyekuwa kaimu katibu mkuu wa Yanga kwa kuwa nafasi hiyo imempata mwenyewe ambaye ni Charles Boniface Mkwasa aliyetangazwa rasmi jana na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.

LISTI YA WALIOKATWA YANGA:
1. Jerry Cornel Muro   (Mawasiliano)
2. Faidhal Mike  (Fedha)
3. Omar Kaya   (Masoko)
4. Sengo Gabriel (Masijali)
5. Heri Juma (Ulinzi)
6. Subira Khalfan   (Usafi)
7. Fatuma Sultan   (Usafi)
8. Ndukane Ally     (Usafi)
9. Rukia Salum      (Usafi)
10. Maneno Hussein   (Usafi)
11. Farijala Kassim     (Usafi)

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic