February 1, 2017

Mashabiki wa eneo la Tunduru wamekaa barabarani na kulizuia basi la wachezaji wa Simba lililokuwa safarini kwenda mkoani Ruvuma.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Polisi wa Tunduru, amelazimika kufika katika eneo hilo akiongozana na askari ambao walifanya kazi ya kuwaondoa mashabiki hao wa Simba, ili wairuhusu Simba kwenda mjini Songea kuivaa Majimaji.

Mashabiki hao walikuwa na hamu ya kuwaona wachezaji mbalimbali huku wakiwasisitiza kwamba wanawaunga mkono na bado wana nafasi ya kubeba ubingwa.

Takribani saa zima, mashabiki waliendelea kuimba na kuwasihi wachezaji wakawachakaze Majimaji na kuendelea kupambana kuwania ubingwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV