February 25, 2017




MPIRA UMEKWISHAAAAAAAA
-Mavugo naye yuko chini hapa, daktari anaingia na kutoka naye nje
-Kichuya yuko chini pale, lakini anainuka 

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89 sasa, Yanga wako kwenye presha kubwa hapa na nje inaonekana mashabiki wameanza kuanguka wakizimia na watu wa huduma wamafanya kazi yao
Dk 86, Mavugo anawatoka mabeki wanne wa Yanga na kuachia mkwaju mkali hapa. Unagonga mtambaa wa panya na kurudi uwanjani
Dk 85 sasa, Simba wanaonekana kutulia zaidi huku Yanga wakiwa na presha ya kutaka kusawazisha
GOOOOOOO Dk 81, Kichuya anafunga bao maridadi kabisa hapa dhidi ya Yanga
Dk 79, Simba wanaingia vizuri tena lakini Yondani anautoa mpira na kuwa kona. Anaichonga Kichuya lakini inaokolewa na kuwa mpira wa kurushwa


Dk 78, Kichuya anapokea pasi ya Mavugo na kuachia shuti kali lakini juuuu
SUB Dk 78, Yanga wanamtoa Zulu na nafasi yake inachukuliwa na Juma Mahadhi 
KADI Dk 77, Niyonzima analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Kotei lakini picha zinaonyesha alijikwaa lakini mwamuzi hakuona vizuri
Dk 77, Yanga wanaonekana kuanza kuupoza mpira lakini wakifanya mashambulizi ya kushitukiza Dk 75 sasa, Simba wanaonekana kucharuka zaidi na kucheza mpira zaidi huku Kichuya, Ajibu na Mavugo wakiwasumbua mabeki wa Yanga
Dk 72, Yanga wanakwenda vizuri na krosi ya MSuva inazuliwa na Kichuya na kuwa kona
SUB Dk 70, Yanga wanamtoa Tambwe, anaingia Deus Kaseke
GOOOOOOO Dk 66 Mavugo anafunga bao safi la kichwa akiunganisha krosi ya Kichuya
Dk 64, Simba wanagongeana vizuri tena ndani ya boksi, wanatoa nje ya boksi na Ajibu anaachia mkwaju hapa lakini unaishia mikononi mwa Dida


Dk Dk 63 Agyei analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Msuva lakini mwamuzi hakuona, anasema goal kick
DK 60, Yanga wanagongeana vizuri, pasi ya Tambwe kwa Msuva lakini Agye anadaka vizuri
SUB Dk 57, Simba wanamtoa Mo Ibrahim na nafasi yake inachukuliwa na Jonas Mkude
Dk 56 Agyei anaudaka mpira wa adhabu vizuri kabisa na Simba wanakwenda kushambulia na kupata kona baada ya Yondani kuutoa nje
KADI Dk 55 Boukungu anamuangusha Chirwa akiwa amebaki peke yake nje ya eneo la hatari, anatolewa nje
Dk 53, Msuva anageuka vizuri kwenye boksi la Simba na kuachia mkwaju mkali kabisa, GOAL KICK
Dk 53, Banda analazimika kufanya kazi ya ziada na kuwa kona


KADI Dk 52, Vicent analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Mavugo
SUB Dk 51, Simba wanamtoa Lufunga na nafasi yake inachukuliwa na Kichuya
Dk 50, Yanga wanapata kona baada ya Lufunga kuutoa mpira nje
Dk 50 Simba wanafanya masihara, krosi ya MWinyi lakini kipa Agyei anawahi na kudaka

Dk 49, Simba wanagongeana vizuri kweli lakini Mavugo aliyetoka kwa kasi anakuwa ni offside
Dk 47, Simba wanaingia vziuri, Mavugo, Mo Ibrahim wanagongeana vizuri lakini mwisho Yanga wanaokoa
Dk 46, Ajibu anamtoka Andrew hapa lakini krosi yake inaishia mikononi mwa Dida
Dk 45 Simba wanaanza kwa kasi na wanakuwa wa kwanza kufika langoni mwa Yanga, lakini Dida anakuwa amini


MAPUMZIKOOO-SUB...Makapu anaingia kuchukua nafasi ya Kamusoko
-Said Juma Makapu anaonekana akipasha hapa, huenda akachukua nafasi ya Kamusoko
- Kamusoko anakaa chini, watu wa hduma ya kwanza wanaingia na kumtoa nje, inaonekana hataingia

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 45, Ajib anapiga mkwaju huo wa faulo lakini ni goal kick hapa
Dk 44, Vicent anamuangusha Mo Ibrahim ndani ya eneo la hatari, lakini mwamuzi anasema ilikuwa nje. Wachezaji wa Simba wanamzonga mwamuzi Mathew Akrama hapa
Dk 43, Kamusoko yuko chini hapa baada ya kugongana na Muzamiru
Dk 42, Kamusoko anaachia shuti kali kimo cha nyoka lakini mpira unatoka nje kidogo
Dk 42, Simba wanagongeana vizuri ndani ya lango la Yanga lakini bado wanashida ya umaliziaji
Dk 40, Mo Ibrahim, anamchambua Kamusoko, anakwenda na kuachia mkwaju mkali kabisa. Dida anadaka, anaachia, anadaka vizuri tena
Dk 38, Agyei tena anauwahi mpira mbele ya miguu ya MSuva, ni baada ya pasi safi ya Kamusoko
Dk 37 Ndemla anaachia fataki kali kabisa hapa lakini inatoka sentimeta chache juu ya lango la Yanga


Dk 37, Agyei anafanya kazi nyingine ya ziada anajitokeza na kudaka vizuri mbele ya Tambwe
Dk 35, nafasi nzuri ya kufunga kwa Simba lakini Ndemla anapaisha juuuuuu
Dk 34, Dida anabaki na mpira muda mrefu na mwamuzi anaweka faulo ndani ya boksi la Yanga
Dk 32, Mavug tena ndani ya msitu wa mabeki wa Yanga, anajaribu kupiga lakini YOndani anazuia na kipa Dida anadaka
Dk 29, nafasi nzuri zaidi kwa Simba, Mavugo akiwa amebaki yeye peke yake na kipa Dida, lakini anapiga nje
Dk 27, hadi sasa Simba wamefanya madhambi mara 6 na Yanga wamefanya mara 4 tu
SUB Dk 27, Simba wanamtoa Liuzio na nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla


Dk 26, Kamusoko yuko chini baada ya kugongana Dk 25, Kamusoko anajaribu shuti la mbali lakini inaonekana ni "chakula" kwa Agyei
Dk 23, Niyonzima anachonga kona nzuri hapa lakini Agyei anaruka na kupangua
Dk 23, krosi safi ya Juma Abdul, Zimbwe anaokoa na kuwa kona ya kwanza
Dk 22, Kotei anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira miguuni kwa Msuva
Dk 21, Yanga wanaingia vizuri hapa, Niyonzima anaachia mkwaju lakini Agyei anadaka kwa ulaini
Dk 18, Simba wanagongeana vizuri tena lakini wamefika mbele, hakuna mipango maridadi
Dk 17, Yondani yuko chini baada ya kugongana na kipa wake
Dk 16, Simba wanagongeana vizuri lakini pasi ya mwisho ya Liuzio, mwamuzi anasema alikuwa ameotea tayari, jambo ambalo ni sahihi


Dk 14, Simba wanagongeana vizuri lakini kinachoonekana hakuna utulivu katika safu ya ushambulizi mbele
Dk 13, Mavugo anakosea kuumiliki mpira karibu kabisa na lango la Yanga na kipa Dida anatokea vizuri na kudaka
Dk 12, mipango ya Simba inaendelea kuonekana ni dhaifu kabisa hasa wanapokaribia upande wa lango la Yanga ambao sasa wanaonekana kujiamini  na kucheza soka safi
Dk 10 sasa, Yanga ndiyo wanaonekana kuuthibiti mpira vizuri zaidi na Simba ni kama hawajiamini huku Lufunga akionekana kama ni mtu aliyechanganyikiwa hivi

Dk 7, Simba wanaonekana kugongeana vizuri kabisa, lakini Yanga wako makini katika safu yao ya ulinzi
GOOOOOOOOOO DK 5, MSuva anaindikia Yanga bao kwa mkwaju safi wa penalti
KADI Dk 4, Mathew Akrama anamlamba kadi ya njano Lufunga kwa kumuangusha Chirwa
PENAAAAT Dk 3, Yanga wanapata penalti baada ya Lufunga kumuangusha Chirwa
Dk 1, Simba wanaonekana kuanza kwa kasi na wanakuwa wa kwanza kufika upande wa Yanga

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic