Ushindi wa Anthony Joshua dhidi ya mkongwe Wladimir Klitschko katika pambano kali la ngumi za kulipwa, imemuingizia kitita cha pauni milioni 15.
Kitita hicho maana yake ni Sh bilioni 42.6 ambazo ameingiza kwa usiku huo mmoja.
Pambano kati ya mabondia hao lilisubiriwa kwa hamu kubwa na lilikuwa ni la kukata na shoka kwa kuwa ilikuwa ni ngumi jiwe raundi ya kwanza hadi 11 lilipofikia tamati kwa Joshua kushinda kwa TKO.
0 COMMENTS:
Post a Comment