April 30, 2017



Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema wao wanaisubiri timu yoyote itakayotinga fainali ya Kombe la Shirikisho.

Tayari Simba imefuzu katika fainali ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza baada kuitwanga Azam FC kwa bao 1-0, jana.

Majanya amesema wanajua watacheza fainali na Yanga au Mbao FC, hivyo hawana sababu ya kuchagua mshiriki.

"Sisi kazi yetu ni kucheza soka, kikosi chetu kitajiandaa na yoyote, awe Yanga au Mbao, tunasubiri," alisema.

Msimu uliopita katika Kombe la Shirikisho, fainali ilikuwa ni kati ya Yanga dhidi ya Azam FC na mechi ikaisha kwa vijana wa Jangwani kubea kombe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic