April 11, 2017Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema Yanga wanajivuruga kwa kuingilia mambo yasiyowahusu.

Kaburu amesema amekuwa akishangazwa na Yanga kuendelea kulivalia njuga suala la Simba kukata rufaa dhidi ya Kagera Sugar.

"Simba imeikatia rufaa Kagera Sugar, Yanga kelele za nini. Hili si suala la nani anasaidiwa na tatizo lipi? Si inajulikana kuwa baada ya kadi tatu za njano nini kinafuatia.

"Kagera sio Yanga, pia kanuni ziko wazi. Hivyo nawashauri waendelee na mambo yao waachane na Simba," alisema Kaburu.

Yanga imekuwa ikilalama kuhusiana uamuzi wa Simba kukata rufaa ikipinga Kagera Sugar kumchezesha beki Mohamed Fakhi ikidai alikuwa na kadi tatu za njano.

Katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Bukoba wiki iliyopita, Simba ilitwangwa kwa mabao 2-1 na wenyeji wake Kagera Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV