April 13, 2017





Wakati Lionel Messi alipoingia uwanjani juzi, alikuwa ana mabao 97 aliyofunga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mpinzani wake, Cristiano Ronaldo, yeye alikuwa na mabao 98.

Kila mmoja alitaka kushindana na mwenzake kuwa wa kwanza kuigusa 100.




Barcelona walifungwa mabao 3-0 na Juventus ya Italia, hivyo Messi akabaki na mabao yake 97. Jana ikawa ni zamu ya Ronaldo ambaye amebadilisha namba.

Ronaldo amefunga mabao mawili wakati Real Madrid ikiiangukia Bayern Munich kwao Munich kwa kuichapa mabao 2-1.

Maana yake, Mreno huyo sasa ana mabao 100 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo ameyafunga akiwa na Manchester United na Real Madrid.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic