April 21, 2017




Meneja wa kiungo mshambualiaji wa Simba, Hija Uganda amelalama kwamba kitendo cha Kocha Joseph Omog kutompa nafasi ya kucheza mchezaji wake ni kuua kipaji chake.


Meneja wa Ugando, Jamali Kisongo amesema kuwa kitendo cha mchezaji huyo kukosa nafasi ya kucheza chini ya Omog, kimekuwa hakimfurahishi ndipo alipoamua kuchukua uamuzi huo wa kutaka aondoke zake klabu hapo ili akatafute maisha sehemu nyingine ambako atakuwa akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

“Kwa mchezaji anayejitambua hata siku moja hafurahii kukaa benchi bila ya kucheza, Ugando kwa sasa maisha yake ndani ya Simba siyo mazuri hapati nafasi ya kucheza jambo ambalo linaweza kuua kipaji chake.


“Kutokana na hali hiyo, hivi sasa nipo katika mazungumzo na uongozi wa Simba ili baada ya msimu huu uweze kumuachia akatafute maisha sehemu nyingine ambako atapata nafasi ya kucheza ili aweze kuinua kipaji chake,” alisema Kisongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic