April 12, 2017



Kocha wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon, ameweka wazi kwamba kitendo cha wachezaji wake kushinda mechi dhidi ya Mbao kilimshangaza hata yeye kutokana na kuamini mechi hiyo ingeisha kwa sare au kupoteza.


Omog kwa mara ya kwanza alivunja mwiko wa Simba kushinda Uwanja wa Kirumba baada ya kupita miaka saba mfululizo bila, walipopata ushindi mbele ya Mbao kwa mabao 3-2.

Kocha huyo amesema kuwa mechi hiyo ni miongoni mwa mechi ngumu ambazo amewahi kukutana nazo akifundisha soka kwani huwa ngumu kwa timu ambayo imefungwa mabao mawili kuweza kupindua matokeo.

“Sikuwa na imani kubwa ya kushinda baada ya kufungwa yale mabao mawili japo nilitambua tuna nafasi ya kushinda kwa sababu sisi tuna uzoefu zaidi ya wapinzani wetu ambao walikuja kuchoka katika dakika za mwisho na sisi ndiyo tukapata mabao yetu.

“Ila niwapongeze Mbao kwa ushindani ambao wametuonyesha na niseme hii ni moja ya mechi ngumu ambazo nimekutana nazo kwenye maisha yangu ya soka kwani kutoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda siyo jambo dogo hata kidogo.


“Sasa tumekaa kwenye uongozi wa ligi na niseme kwamba hiki tulichokifanya mbele ya Mbao ndiyo tutakifanya kwenye mechi nyingine zijazo ikiwemo mchezo wetu dhidi ya Toto,” alisema Omog.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic