SportPesa ni watu wanaokwenda na utekelezaji wa ahadi yao baada ya haraka kutimiza ahadi yao ya kutoa kitita cha Sh milioni 50 kwa kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys.
SportPesa walitoa ahadi hiyo wakati wa uzinduzi wao juzi na leo wamekabidhi rasmi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwanyembe.
Abbas Tarimba ambao ni mmoja wa Wakurugenzi wa SportPesa Tanzania, ndiye alimkabidhi mfano wa hundi hiyo Dk Mwakyembe leo hii mchana.
Awali Dk Mwakyembe alieleza kufurahishwa na fursa ya SportPesa na kusema hatailazia damu kwa kuwa angependa kuona michezo inaungwa mkono.
0 COMMENTS:
Post a Comment