May 1, 2017


Kazi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali inaanza kesho.

Real Madrid watakuwa nyumbani dhidi ya jirani zao Atletico Madrid.

Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu inasubiriwa kwa hamu kubwa.

Madrid wakiongozwa na Kocha Zinedine Zidane na nyota wao Cristiano Ronaldo, wameonekana wako tayari kwa mechi ya keshii.

Hata hivyo, haitakuwa mechi laini hata kidogo na watalazimika kufanya kazi ya ziada ili kujiweka vizuri kabla ya mechi ya pili kwenye Uwanja wa Vincete Calderon.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV