May 12, 2017




Timu ya Stand United ya Shinyanga, imetamba kumsimamisha Mnyama leo Ijumaa wakati timu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Taifa, Dar huku Simba ikilazimika kushinda ili kuendeleza matumaini yake ya kutwaa ubingwa huo msimu huu.

Stand United inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, imejipanga vilivyo kuwasimamisha Simba waliopo nafasi ya pili ambao wanakimbizana na Yanga kuwania ubingwa.

Ofisa Habari wa Stand United, Deokaji Makomba, amesema kuwa japokuwa walikumbwa na changamoto ndogondogo za kiuchumi kipindi cha mzunguko wa kwanza ila sasa wamejipanga vizuri kuondoka na pointi tatu kwani ni muhimu kwao.

“Hali ya vijana ipo vizuri na kila mchezaji amejipanga kuwakabili Simba, tunajua mchezo huu utakuwa wa vuta nikuvute, sisi tunazitaka pointi tatu na hata wapinzani wetu hivyohivyo wanazitaka pointi hizo, lakini kwa jinsi tulivyojipanga ni lazima tuwasimamishe Simba kwa kuwachapa,” alisema Makomba. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic