May 11, 2017



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwanyembe amesema serikali itashirikiana na watu walio tayari kusaidia masuala mbalimbali ya michezo kama ilivyo kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa.

Dk Mwanyembe amesema uamuzi wa SportPesa kuanza kwa kusaidia jamii hasa katika michezo, ni jambo wanalolichukulia kwa uzito au fursa.

“Sisi tutawaunga mkono SportPesa katika jitihada zao. Lengo lengo ni watusaidie kuendeleza vijana na kupata akina Mbwana Samatta wengi,” alisema.



“Tunachotaka ni kuwaendeleza zaidi na SportPesa ni kuwaendeleza zaidi,” alisema.

Wakati wa uzinduzi, SportPesa walitoa kitita cha Sh milioni 50 kusaidia juhudi za Serengeti Boys kufanya vizuri katika mechi za Kombe la Mataifa Afrika nchini Gabon.

Tayari kampuni ya SportPesa imezinduliwa hapa nchini na imeanza kufanya shughuliz ake.

Kabla kampuni hiyo ilikuwa ikifanya kazi zake nchini Kenya na imefanikiwa kufanya udhamini katika timu kongwe za AFC Leopards na Gor Mahia pia Nakuru All Stars.


Kama haitoshi imeeinua Ligi Kuu ya Kenya na sasa imekuwa na umaarufu kutokana na kuwa na udhamini mkubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic