May 4, 2017


Timu kadhaa za Ulaya zikiwemo nyingi ambazo ni vigogo zimeelekeza macho na nguvu zake nyingi kwa wachezaji wa kikosi cha Monaco.

Monaco imefanikiwa kuingia kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku ikionekana kuwashangaza wengi.
Hali hiyo imefanya vigogo wengi kuanza kuwafuatilia wachezaji wao.

Tiemoue Bakayoko (Kiungo, 22)
Anatakiwa na: Chelsea

Fabinho (kiungo/beki wa kulia, 23)
Anatakiwa na: Manchester United, Barcelona

Thomas Lemar (kiungo mshambulizi, 21)
Anatakiwa na:  Tottenham Hotspur, Chelsea

Kylian Mbappe (mshambuliaji, 18) 
Anatakiwa na:  Real Madrid, Barcelona, Chelsea, Arsenal

Djibril Sidibe (beki wa pembeni, 24) 
Anatakiwa na:  Arsenal, Chelsea

Bernardo Silva (kiungo mshambuliaji, 22)
Anatakiwa na:  Manchester United, Barcelona, Real Madrid

Benjamin Mendy (beki wa kushoto, 22)
Anatakiwa na:  Manchester City, Manchester United


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV