June 19, 2017Baada ya uongozi wa Simba kumtangaza beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuwa mchezaji bora wa msimu kwa timu hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kuwa atamchagua mchezaji wake bora anayemtaka na kumpa zawadi ya gari.

Msimu uliopita Poppe alimchagua beki huyo na kumzawadia gari aina ya Toyota Raum ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi na mchango wake kwa timu hiyo.

 Poppe amesema kuwa mchezaji aliyechaguliwa na uongozi wa timu hiyo na kutunukiwa tuzo, hahusiani na mchezaji aliyepanga kumchagua  na kumpa zawadi hiyo ya gari.

“Tshabalala amechaguliwa na Simba kama mchezaji bora wa msimu, binafsi kwa upande wangu bado sijamchagua mchezaji ambaye nitamzawadia gari ambayo nimepanga kutoa kama nilivyofanya msimu uliopita.

“Muda bado upo wa kutosha  kwa sababu hata huyo Tshabalala nilimchagua  peke yangu bila kumshirikisha mtu yeyote na kweli leo kila mmoja nadhani anaona ubora wake, sasa hata kwa ambaye nitamchagua naamini atakuwa bora kutokana na jinsi alivyojituma, atabaki kuwa siri kwa sasa mpaka hapo nitakapoitoa hiyo zawadi katika Simba Day,” alisema Poppe.1 COMMENTS:

  1. ni KICHUYA kwa kuwa kawafunga yanga mara mbili, kafunga goli linalo ifanya simba ishiriki kombe la washindi afrika

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV