June 11, 2017Beki mkongwe, Besala Boukungu ni sawa na “home work” kwa kamati ya usajili na ile ya ufundi ya Simba.


Kwamba abaki au aende, hakuna ambaye ana uhakika wa asilimia kwa kuwa kuna mambo yanachanganya.

Imeelezwa kati ya wajumbe, wako wanaona wakati umefika aende na wengine wanaona angalau msimu mmoja aongezewe.

“Unajua kweli umri wa Boukungu umekwenda, lakini alionyesha weledi sana. Uwanjani alijituma na nje ya uwanja alikuwa ni profesional kabisa,” kilieleza chanzo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, yeye alisema kazi ya Boukungu alikuwa bora na wanaona atabaki.


Lakini kuna viongozi wanaamini vizuri wakamruhusu kwa heshima na kumpongeza kwa kazi yake nzuri ili aondoke.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV