June 17, 2017Klabu ya Singida United imefanikiwa kumsajili mshambuliaji hatari wa Polisi ya Rwanda na timu ya taifa ya nchini hiyo 'Amavubi' au Manyigu.

Singida imemsajili Danny Usengimana kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Polisi.

Usengimana ndiye mfungaji bora misimu miwili mfululizo, alikuwa mfungaji bora msimu uliopita lakini akarudia tena msimu huu baada ya kutundika nyavuni mabao 19.

Singida United iliyopanda daraja msimu huu imekuwa ikisidi kujiimarisha katika kila idara huku ikisajili wachezaji wa kimataifa wakiwemo wale kutoka Zimbabwe.

Kikosi cha Singida United kinaongozwa na Kocha Hans van der Pluijm ambaye amebeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara akiwa na Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV