June 16, 2017Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kukutana na mshambuliaji, Emmanuel Okwi na kufanya naye mazungumzo.

Mazungumzo ya Okwi na Hans Poppe yamefanyika katika hoteli ya Serena jijini Kampala, leo.

Hans Poppe amezungumza na SALEHJEMBE na kusema, yalikuwa ni mazungumzo yenye mafanikio.

“Yalikuwa mazungumzo yenye mafanikio, tumezungumza vizuri na tumemalizana vizuri. Baada ya hapo unajua zoezi linalofuatia,” alisema Hans Poppe.

Hans Poppe ambaye ni askari wa jeshi mstaafu, amesema Okwi atakuja Dar es Salaam hivi karibuni.

“Hayo mengine tuyaache, ila Okwi atakuja Dar es Salaam hivi karibuni.”

Hivi karibuni, Okwi alizungumza na SALEHJEMBE alisema atakuja nchini Tanzania na alikuwa tayari.

Hata hivyo alisisitiza kwamba hakuwa amefanya mazungumzo ya kina na uongozi wa Simba zaidi ya kujua kama wanamhitaji.


Lakini inavyoonekana, mazungumzo ya kina yatakuwa yamefanyika leo na baadaye picha zilianza kusambaa mtandaoni, akiwa na Hans Poppe.

3 COMMENTS:

 1. Tatizo la Hans na wenziwe wanawafanya wanachama wa Simba hawana akili,mwanzo walisema wameshamalizana na Okwi,Leo tena anapiga nae picha wapo Uganda wanafanya mazungumzo,sarakasi zenu ndizo zinazowadondosha tafuteni wachezaji wa maana waje kuisadia timu,msisajili kwa historia mtapotea hakikisheni waxhezaji wenu wazuri wanabaki klabuni,hiyo itawasaidia kuwa na timu imara yenye WACHEZAO waliokaa pamoja kwa muda mwingi.Hasara mnayoitafuta ndiyo waliyoipata Yanga kwa Zulu,ni mchezaji mzuri aliye kosa kucheza kwa muda mrefu matokeo yake akakosa kujiamini uwanjani kisha akakosa kuaminiwa na kocha Mwisho wa siku hakuwa chaguo la kwanza la kocha,na hiyo siyo nzuri kwa mchezaji wa kigeni.Nionavyo mimi Simba inaweza kupata wachezaji waziri wa humu ndani na wenye msaada kwa timu kuliko Okwi ambaye atapewa pesa nyingi kisha anakaa benchi.VIONGOZI WA SIMBA SAJILINI KWA KUFUATA MAPENDEKEZO YA BENCHI LA UFUNDI.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Upo sahihi hawa ni watu wa dili na kuuza sura tuu ktk magazeti. Huyu alitakiwa akae pembeni miaka yote hii wanasajili magarasa na yatarembwa sana na waandishi njaa, ikifika muda watavunja mkataba kuwa eti kaisha na kulipana mamilioni ambayo tena wanaishia kugawana..

   Ndiyo maana badala ya kusajili wacheaji wazuri, wadogo wa hapa lazima wakimbilie wazee wa nje kila kukicha. Kwa nn tusingesajili angalau 4-5 wa serengeti boys na kubakiza wengi waliopo ili kujazia mapengo?
   Ona upuuzi walioufanya dirisha dogo ?

   Sasa leo tunajaza viungo wa nn wakati wamejaa kibao? Hata hao makanjanja wa yanga na azam wa nn, keho tukifungwa mtaibuka kuwa wameuza !!Hivi hao mtibwa, au hata Mbao wao wana macho gani ambayo nyie hamna kila mwaka kuibua vijana wazuri wa hapa nyumbani ?

   Nneweka rekodi ya kuwa viongozi wa ovyo kuwahi kutokea!

   Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV