June 18, 2017Jonas Mkude amebaki Simba lakini atakuwa ndiye mchezaji anayelipwa kitita kikubwa zaidi kwa maana ya mshahara kwa wazawa.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zinaeleza, Mkude atakuwa akichukua Sh 5,000,000 kwa mwezi.

Kama utafanya hesabu kwa mwaka, maana yake Mkude atakuwa akiingiza Sh milioni 60 kwa mwaka, kwa mshahara pekee.

Lakini bado atakuwa akitegemea posho au bonus kutokana na kikosi chake kinavyofanya vizuri.

Nahodha huyo wa Simba, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba.

Mkataba huo umesainiwa jana na kuhitimisha mbio za Yanga kumuwania Mkude kujiunga na timu hiyo yenye makao yake makuu Jangwani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV