June 18, 2017






Taarifa za usajili wa kiungo Haruna Niyonzima, zimeendelea kuzua mjadala mkubwa mtandaoni.

Kuna wanaosema kasaini Simba na wengine wanadai ameongeza mkataba Yanga.

Habari kutoka kwa rafiki wa Niyonzima, zimeeleza hadi sasa kiungo huyo Mnyarwanda hajasaini upande wowote.

“Niyonzima hajasaini Simba wala Yanga, haya ni maneno tu ya watu ndugu yangu.  Lakini tutajua baadaye au siku nyingine,” kilieleza chanzo.

Niyonzima amekuwa akiwaniwa na Simba baada ya kuichezea Yanga kwa misimu sita akitokea APR ya Rwanda.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic