July 5, 2017

Washtakiwa wengine ambao wapo kwenye kesi moja na Manji wakiwa kwenye karandinga la polisi.

Wimbi la vigogo wa ngazi na hadhi mbalimbali kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali limeendelea baada ya leo Julai 5, 2017, mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji kusomewa shitaka la uhujumu na kunyimwa dhamana.


Manji amesomewa na wenzake wanne wamesomewa hayo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam kwa kuwa Manji alikuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa moyo.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, wengine walipelekwa rumande na Manji akabaki hospitali ambako anaendelea kupatiwa matibabu.


Waendesha mashtaka wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam, ilihamia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako Manji amelazwa na kusomewa mashtaka saba, ambayo kukutwa na kukutwa na bidhaa visivyo halali, ambavyo ni vitambaa vyenye thamani ya shilingi milioni 44, ambavyo ni mahususi kwa ajili ya kutengeneza sare za JWTZ.

Watuhumiwa hao wamekutwa na mihuli miwili ya JWTZ wa kwanza ni wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, Muhuli wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na mhuri mwingine wa Commanding Officer Korogwe, plate number 2 za magari ya serikali yanayowakabili washtakiwa wanne akiwemo Manji.


Pia washtakiwa wamekutwa na shitaka la kukutwa na mihuli ya Jeshi la Wananchi Kambi ya Makutupola, Dodoma Kambi namba 834 jambo ambalo ni kinyume cha sheria.




Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja na watuhumiwa wote wamenyimwa dhamana.



Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 19 mwaka huu ambapo itasomwa tena huku Manji akiendelea kutibiwa Muhimbili chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic