July 5, 2017


FULL TIME 

Mwamuzi anamaliza mchezo, Tanzania inatolewa kwa jumla ya mabao 4-2. 

Dakika ya 93: Muda wowote kuanzia sasa mchezo utamalizika.

Dakika ya 92: Kuna Watanzania wanashangilia wakiwa jukwaani

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.


Dakika ya 89: Stars wanapiga pasi nyingi eneo la katikati ya uwanja lakini zinakuwa hazina faida. Mzamiru ndiye ambaye anaonekana muda mwingia kipiga pasi.

Dakika ya 86: Msuva anapata nafasi nyingine lakini shuti kali lakini linatoka nje.Dakika ya 86: Msuva anapata nafasi nyingine lakini shuti kali lakini linatoka nje.

Dakika ya 83: Simon Msuva anaipatia Taifa Stars bao la pili kwa shuti kali.
 
GOOOOOOOOOOOOOOOOO!

Dakika ya 81: Elius Maguri anatoka,anaingia Thomas Ulimwengu.

Dakika ya 80: Mashabiki wa Tanzania wlaiokuwa wakishangilia kwa nguvu hapa uwanjani wote wamekaa kimya, wengi wao wanajadiliana mambo kadhaa.


Dakika ya 77: Stars wanajaribu kutengeneza mashambulizi lakini inashindikana.

Dakika ya 73: Shomari Kapombe anapoteza mpira na kucheza faulo kwa mshambuliaji wa Zambia.

Dakika ya 70: Zambia wanamiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya 68: Wachezaji wa Stars wanaonekana kupunguza kasi.


Dakika ya 68: GOOOOOOOOOOOOOOOO Shonga anaipatia Zambia bao la nne kutokana na mpira wa faulo, alipiga shuti kali likaelekewa wavuni moja kwa moja.

Dakika ya 56: GOOOOOOOOO Zambia wanapata bao la tatu kwa njia ya penalti.

Dakika ya 50: Mchezo unaendelea kwa kasi

Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO

Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.

Walinzi wa Taifa Stars wanafanya uzembe, mfungaji yuleyule wa bao la kwanza anaipatia Zambia bao la pili baada ya kupita katikati ya mabeki.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.

Dakika ya 45: Stars wanafanya mabadiliko, anatoka Nyoni ambaye ameumia mguu, anaingia Rafael Alfa.

Zambia wanasawazisha bao kupitia kwa Briana Mwila baada ya kupigwa pasi ndefu kisha mfungaji akabaki yeye na kipa, akauweka mpira wavuni akiunganisha krosi iliyotoka upande wa kulia.

Dakika ya 43: GOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 40: Taifa Stars wanapata kona tatu mfululizo lakini wanashindwa kuzitumia vizuri.

Dakika ya 39: Kichuya anapiga faulo nzuri lakini kipa wa Zambia anaipangua inakuwa kona.

Dakika ya 38: Msuva anachezewa faulo nje ya eneo la 18 na kusababisha beki wa Zambia apate kadi ya njano.

Dakika ya 36: Mchezo una ushindani, kipa wa Stars, Aishi Manula anawaelekeza walinzi wake kujipanga vizuri.

Dakika ya 34: Shuti kali linapigwa kwenye lango la Stars, linagonga nguzo ya juu baad aya mabeki wa Stars kuwa wazembe, inakuwa kona.


Dakika ya 30: Zambia wanaendelea kutengeneza mazingira kupitia pembeni lakini inakuwa ngumu.

Dakika ya 27: Kasi ya mchezo imeongezea, Zambia wanatengeneza mashambulizi lakini walizni wa Stars wanakuwa makini.

Dakika ya 24: Nyoni ameumia, amekaa chini, mchezo umesimama kwa muda, ababebwa kwenye machela anatolewa nje kisha mchezo unaendelea.

Dakika ya 20: Kasi ya mchezo imeongezeka.

Dakika ya 18: Stars wanaendelea kulishambulia lango la Zambia.

Dakika ya 15: Stars wanafika tena langoni mwa Zambia lakini Msuva anakuwa ameotea.

Dakika ya 14: Erasto Nyoni anaipatia Taifa Stars bao kwa njia ya shuti la faulo. Amepiga shuti limejaa moja kwa moja wavuni. 

GOOOOOOOOOOOOO!!!!!!

Dakika ya 13: Simon Msuva anachezewa faulo nje ya eneo la 18 la Zambia. Mwamuzi anaamuru ipigwe faulo.

Dakika ya 10: Bado timu zote zinasomana taratibu.

Dakika ya 4: Tanzania wanafika langoni mwa Zambia wanafanya shambuliai la nguvu lakini wanakosa nafasi.

Dakika ya 2: Mchezo umeanza kwa kasi ndogo

Mwamuzi ameanzisha mchezo

Taifa Stars ipo uwanjani kuivaa Zambia katika nusu fainali ya COSAFA, inayoendelea nchini Afrika Kusini, ikiwa imefika hatua hiyo baada ya kuwatoa wenyeji ambao pia walikuwa mabingwa watetezi, Afrika Kusini kwa ba 1-0, bao likifungwa na mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 17.

Kikosi cha Taifa Stars hiki hapa…
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Gadiel Michael
4. Salim Mbonde
5. Abdi Banda
6. Erasto Nyoni
7. Himid Mao
8. Muzamiru Yassin
9. Simon Msuva
10. Elius Maguri
11. Shiza Kichuya

Waliopo benchi
1. Said Mohamed
2. Hassan Kessy
3. Amim Abdulkarim
4. Nurdin Chona
5. Salmin Hoza
6. Rafael Daud
7. Thomas Ulimwengu
8. Stamil Mbonde

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV