July 20, 2017


Kikosi cha Mbeya City kimeanika jezi zake mpya lakini kikiwa kimechukua ushauri iliotolewa na Salehjembe kutoa msalaba kwenye jezi zao.

Awali Mbeya City walionyesha hadharani jezi ziliokuwa na alama ya msalaba na blog hii ikawapa ushauri kuachana na mfumo huo mara moja kwa kuwa timu za Tanzania si sawa na zile za Ulaya.

Pia kufanya hivyo ni sawa na kuwachanganya mashabiki ambao wanapokuwa katika timu wanakuwa hawana dini.

Safari hii wametangaza jezi zao mpya zikiwa na chata ya mdhamini RB Battery, jambo ambalo linaonyesha ni watu wanaofuata weledi.

Kingine kizuri katika jezi hizo zinaonekana kutokuwa na mambo mengi kama ambavyo inatakiwa katika jezi nyingi za kisasa.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic