July 19, 2017

MGETA WA PILI KULIA MBELE WALIOKAA, AKIWA NA KIKOSI CHA VBF EPPINGEN AMBACHO AMEJIUNGA NACHO HIVI KARIBUNI.

Mtanzania Emily Mgeta ameanza kazi ya kujifua VfB Eppingen ya nchini Ujerumani.

Mgeta amejiunga na timu hiyo ya daraja la tano nchini Ujerumani akitokea Neckarsulmer ya daraja hilo pia.

Akizungumza kutoka nchini humo, Mgeta aliyewahi kuichezea Simba amesema wameanza mazoezi.

“Tumeanza kujifua na nimeanza kuzoeana na wenzangu,” alisema.

“Awali nilikuwa mgeni lakini sasa nimeanza kuzoea na mambo ninaamini yatakwenda vizuri.”


Mgeta aliyekulia kisoka mkoani Mwanza, aliwahi kuichezea Simba katika kikosi cha vijana na baadaye akacheza Polisi Moro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic