July 29, 2017




SIMBA SPORTS CLUB 
DAR ES SALAAM 
29-7-2017




 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
______________ 


Benchi la ufundi la klabu ya Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu. 

Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu,beki wa kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba,akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi hicho,ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika kusini kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao. 

Kwenye mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu,Mohammed Hussein(Tshabalala)na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo. 

Klabu inamshukuru sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake mwandamizi,Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa Nahodha wa Timu. 

Kwa sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema huko kambini Eden Vale Johannesburg nchini Afrika kusini. 

IMETOLEWA NA.. 

HAJI S MANARA 

MKUU WA HABARI WA SIMBA SC 


SIMBA NGUVU MOJA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic